Wednesday, 11 March 2015

AJALI MBAYA YATOKEA MKOANI IRINGA

Ajali mbaya yatokea maeneo ya Mafinga Iringa sehemu kunaitwa Changarawe ambapo gari aina lori lilokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya ambapo lilikuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara na kugongana na gari la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar.
Kontena la lori limelalia kabisa basi, na watu wengine wamelaliwa na wengine wameporomokea korongoni, mpaka sasa hakuna majeruhi ni maiti tu, wala hakuna mtu ambaye inadhaniwa amepona.
- Kuna watoto wawili wasalimika, makadirio yao ni kati ya miaka mitatu na saba, lakini hawa inasemekana kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo mgongano.

Fuatilia zaidi.


Ajali Mbaya mkoani Iringa_Mafinga.

Zitto Kabwe avuliwa rasmi uanachama Chadema

Kwa ufupi
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
 
Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho…
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Akitangaza hatua hiyo ya kumvua uanachama,Lissu amesema kanuni na sharia za chama hicho ziko wazi na zinaelekeza kuwa endapo mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho mahakamani na iwapo atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama.