Wednesday, 11 March 2015

AJALI MBAYA YATOKEA MKOANI IRINGA

Ajali mbaya yatokea maeneo ya Mafinga Iringa sehemu kunaitwa Changarawe ambapo gari aina lori lilokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya ambapo lilikuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara na kugongana na gari la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar.
Kontena la lori limelalia kabisa basi, na watu wengine wamelaliwa na wengine wameporomokea korongoni, mpaka sasa hakuna majeruhi ni maiti tu, wala hakuna mtu ambaye inadhaniwa amepona.
- Kuna watoto wawili wasalimika, makadirio yao ni kati ya miaka mitatu na saba, lakini hawa inasemekana kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo mgongano.

Fuatilia zaidi.


Ajali Mbaya mkoani Iringa_Mafinga.

0 comments:

Post a Comment